Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 25, 2016

Watu 80 wafariki katika shambulizi la Bomu lililowalenga washiha Iraq

Vyombo vya usalama vya Iraq vimesema kwamba zaidi ya watu themanini wameuawa kwa shambulizi la bomu lililowalenga madhehebu ya kiislamu ya kishia kusini mwa mji wa Baghdad.
Gari lililokuwa limebeba vilipuzi hivyo lililipuka karibu na kituo cha mafuta ambapo watu wengi wa dhehebu hilo walikuwa wameegesha magari yao.
Wengi wa watu waliofariki ni wananchi wa Iran na Afghanistan.
Walikuwa wakitoka kwenye moja ya tukio muhimu la kidini kwenye mji mtakatifu wa Karbala.

Mamia ya washiha hufanya hija katika mji wa Karbala
Image captionMamia ya washiha hufanya hija katika mji wa Karbala

Askari wa kundi la kiislam wamekiri kuhusika na shambulizi hilo.
kundi hilo la wapiganaji la kiislam mara kwa mara hulenga madhehebu ya kishia na kuwatuhumu kwamba ni waongo.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP