wolper-3
Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper akiwa kapozi na gari hilo aina ya Toyota Alphard .
Hamida Hassan na Imelda Mtema, Ijumaa
Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper amenunua gari lenye thamani ya shilingi milioni 20 ambalo kwa sasa anamalizia usajili wake.
listing_main_2014_toyota_alphard_interior_2Muonekano wa ndani wa ndinga yake hiyo mpya.
Ijumaa lilimbabatiza Wolper mitaa ya Kinondoni jijini Dar akiwa na gari hilo aina ya Toyota Alphard ambapo alipobanwa kama amelikodi kama wanavyofanya mastaa wengine au amenunua alifunguka kuwa ni lake kutoka kwenye hela yake halali.
wolper-2Wolper akiwa katika pozi.
“Hii gari ni yangu kama mnavyoiona mpya kabisa, nimeinunua na ndo’ kwanza nashughulikia usajili,” alisema Wolper.
Wolper alisema kuwa anakwepa mambo yaliyompata kwenye ile gari yake iliyomletea matatizo aina ya BMW X-6 ambapo alipata funzo na sasa hawezi kufanya makosa tena.
2008_toyota_alphard_02
Gari aina ya Toyota Alphard.
“Nimeamua nifanye usajili kabisa TRA, sitaki matatizo kabisa kuhusu magari, lile lilinifanya nipate funzo kubwa,” alisema Wolper.
Wolper mbali na kununua gari amefungua duka la nguo Kinondoni. Kufuatia mambo hayo makubwa aliyofanya msanii huyo, wadau walihoji kama mkwanja wa kufanyia yote hayo umetokana na safari ya China au kuna pedeshee kaamua kumpa maisha? Jibu analo mwenyewe.