Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 22, 2016

Zaidi ya wahitimu laki mbili kupata ajira Nigeria

Zaidi ya wahitimu laki mbili nchini Nigeria ambao hawakuwa na ajira wameanza kupokea ujumbe mfupi unaowataarifu kuwa wameajiriwa na mchakato maalumu wa ajira wa serikali.

Wamekuwa ni awamu ya kwanza kupata ajira kati ya waliohitimu kufuatia ahadi ya kutoa ajira kwa zaidi ya wahitimu nusu millioni nchini Nigeria iliyotolewa na serikali katika uchaguzi mkuu mwaka uliopita.
Watakuwa wakilipwa karibia dola millioni mia moja kwa mwezi.
Ofisi ya waziri mkuu imeeleza kwamba zaidi ya wahitimu laki moja katika awamu ya kwanza ni walimu, na wengine laki tatu wataajiriwa katika sekta ya kilimo na watakaobakia watakuwa katika sekta ya Afya.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP