Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Dec 19, 2016

Barua ya Mohammad Ali kwa Mandela yauzwa pauni 7,200

Barua iliyowekwa sahihi na mwanamasumbwi Mohammad Ali na kuandikiwa rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, akitoa rambu ramba zake kufuatia kuawa kwa mtu aliyekuwa akipinga ubaguizi wa rangi imeuzwa kwa pauni 7,200.
Muuzaji wa barua hiyo Andrew Aldridge alisema, "ni vyema kuwa Mohammad Ali alikuwa mwanamichezo bora zaidi hukui naye Nelson Mandela akiwa mtu mashuhuri zaidi katika karne iliyopita.
Barua hiyo ilipiwa chapa cha msaidizi wa meneja wa hoteli ya Elangeni iliyo mjini Durban ambapo Ali alikuwa akiishi wakati huo.
Barua hiyo iliyouzwa kwa mnunuzi kutoka nchini Marekania ilitarajiwa kuuzwa kwa kati ya dola 6,000 na 8,000.
Muhammad Ali alikaa kipindi cha majuma mawili nchini Afrika KusiniImage copyrightAFP
Image captionMuhammad Ali alikaa kipindi cha majuma mawili nchini Afrika Kusini
Chris Hani (kushoto)Image copyrightREUTERS
Image captionChris Hani (kushoto)
Muhammad Ali alikuwa nchini Afrika Kisini kwa kipindi kifupi mwezi Aprili mwaka 1993 baada ya kuwasili muda mfupi baada ya kuuliwa kwa Chris Hani tarehe 10 mwezi Aprili.
Hani alikuwq kamanda wa kundi la Umkhonto We Sizwe, kundi lililojihami la ANC.
Alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya ubaguzi wa rangi na aliuawa mkereketwa mmoja nje ya nyumba yake eneo la Boksburg.
Barua wa Muhammmad Ali kwa MandelaImage copyrightPA
Image captionBarua wa Muhammmad Ali kwa Mandela

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP