Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Dec 21, 2016

Hali ya utulivu yerejea nchini DR Congo

Hali ya utulivu imerejea katika barabara za mji mkuu wa Kinshasa pamoja na zile za miji mingine muhimu nchini DR Congo kufuatia maandamano.
Kiongozi wa upinzini nchini humo Etienne Tshisekedi , amewataka wafuasi wake kuipinga serikali ya rais Joseph Kabila .
Zaidi ya watu 20 wameuawa katika ghasia baada ya muhula wa Kabila kukamilika siku ya Jumatatu usiku huku uchaguzi ukiwa umeahirishwa hadi 2018.
Kanisa katoliki linatarajiwa kuendeleza mazungumzo kati ya upinzani na muungano wa kitaifa.

Maandamano ya kumpinga rais Kabila yalifanyika huku zaidi ya watu 20 wakidaiwa kuuawa na wanajeshi
Image captionMaandamano ya kumpinga rais Kabila yalifanyika huku zaidi ya watu 20 wakidaiwa kuuawa na wanajeshi

Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema kuwa kanisa linaheshimiwa sana nchini humo kwa miongo kadhaa na kwamba mazungumzo hayo huenda yakatuliza hali ya wasiwasi iliopo iwapo upinzani na serikali hawataafikiana

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP