Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Dec 21, 2016

Jamii ya kimataifa yamtaka Kabila kujiuzulu

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila anazidi kupokea shinikizo kimataifa kutokana na hatua ya kukataa kuachia maamlaka baada ya muhula wake wa kikatiba kukamilika jumatatu.

Ufaransa imesema itatuma ombi kwa umoja wa ulaya la kumwekea vikwazo iwapo ataendelea kushikilia maamlaka.Ujerumani imehairisha majadiliano ya kuipa DR Congo msaada wa miradi ya maendeleo.Inaripotiwa kwamba utulivu umerejea nchini humo baada ya kushuhudiwa machafuko Jumatano, ambapo kulingana na Umoja wa Mataifa, takriban watu 20 waliuwawa.
Uchaguzi mkuu ulioratibiwa kufanyika mwaka huu, uliharishwa hadi mwaka 2018

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP