Mwandishi mmoja wa habari kutoka shirika la Reuters anasema kuwa amezungumza na Adama Barrow aabaye amemuambia kuwa anasubiri simu ya kukubali kushindwa kutoka kwa bwana Jammeh.
Image copyrightAFPImage captionYahya Jammeh ameitawala Gambia kwa miaka 22
Waziri wa masuala ya ndani nchini Gambia na mkuu wa polisi wamehutubia taifa wakitaka kuwepo utulivu.
Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Gambia amewaambia waandishi wa habari kuwa Rais Yahya Jammeh ambaye ameitawala nchi kwa miaka 22 baada ya kuingia madarakani kwa njia ya mapinduzi atakubali kushindwa.
0 Comments