Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Dec 20, 2016

Maandamano ya kumtaka Kabila kujiuzulu yafanyika duniani

Kumekuwa na maandamano katika miji kadhaa mikuu duniani ya kumtaka rais wa DR Congo Joseph Kabila kujiuzulu.
Leo ni siku ya mwisho ya utawala wake ,lakini uchaguzi umeahirishwa ambapo upinzani wa taifa hilo unasema kuwa ni jaribio la Kabila kusalia madarakani.

Vikosi vya usalama vikipiga doria katika mji wa kinshasa nchini DR Congo
Image captionVikosi vya usalama vikipiga doria katika mji wa kinshasa nchini DR Congo

Katika mji mkuu wa Kinshasa na kwengineko, kuna idadi kubwa ya vikosi vya usalama na raia wameamua kusalia majumbani mwao.
Takriban watu 40 wamekamatwa katika mji wa mashariki wa Goma.
Mazungumzo na upinzani yanayofanywa na viongozi wa makanisa yamefeli kuafikia mwafaka, jaribio jingine la kuendeleza mazungumzo hayo litaendelea siku ya Jumatano.

Mji wa Kinshasa nchini DR Congo
Image captionMji wa Kinshasa nchini DR Congo

Zaidi ya watu hamsini walifariki katika makabiliano ya barabarani mnamo mwezi Septemba.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP