Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi alikuwa mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo.



na fredy mgunda,iringa


Madiwani wa halmashauri ya
mji wa mafinga wilayani mufindi wameongezewa makali ya kiutendaji  na uwajibikaji na shirika lisilo la
kiserikali la policy forum kutoka jiji Dar es salaam.

Akizungumza na blog hii
mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi alisema kuwa mafunzo wanayopewa
madiwani yanalengo la kuwaongezea uwezo wa utendaji wa kazi katika kata zao.

Aidha Chumi alisema kuwa ili
kupata maendeleo ya halmashauri ya mji wa Mafinga ni lazima madiwani wawe na
uelewa wa kuzishughulikia kero za wanachi na kuwa wabunifu wa kupanga mipango
ya kuleta maendeleo.

“Ukiangalia madiwani wengi
bado hawavijui baadhi ya vitu na kuhoji kutokana na kanuni na sheria za
halmashauri hivyo nimeleta semina hii kuwaongezea uwezo madiwani wa jimbo la
mafinga”.alisema Chumi

Nao baadhi ya madiwani walimshukuru
mbunge wa jimbo la mafinga Cosato Chumi kwa kuwatafutia watu wa kuwapa elimu ya
kiutendaji na kujua majukumu ya madiwani katika kuisimamia miradi ya
halmashauri.

“Angalia tulikuwa hatujui
mambo mengi na ndio chanzo tulikuwa tunamuingilia majukumu mkurugenzi kama
tulikuwa tunakagua barabara za mji wa mafinga kumbe tulikuwa kinyume na
utaratibu”.walisema madiwani wa mafinga

Kwa upande wake meneja
uwajibikaji wa shirika lisilo la kiserikali la policy forum Richard Angelo alisema
kuwa madiwani wengi wanakumbana na changamoto za kuisimamia halmashauri hivyo
wameamua kuwa elimu ya kujua wajibu wao.

Hata hivyo Angelo alisema
kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa madiwani na wabunge karibia wote lengo likwa ni
kukuza uelewa na uwezo wa kuongoza maeneo wanayowaongoza.

“Hivi karibu tumetoa elimu
kwa wabunge mjini Dodoma na ndipo mbunge wa jimbo la Mafinga Cosato Chumi
alituomba tuje kutoa elimu kwa madiwani wa jimbo lake na ndio maana ndio tupo
hapa mjini Mafinga”.alisema Angelo