Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Dec 6, 2016

Mfanyabiashara kizimbani hasara ya mil. 657.5/-

MFANYABIASHARA maarufu wa Jijini Arusha mwenye asili ya kiasia, Firoz Khane (55) amesomewa mashitaka yake ya awali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kwa kosa la kuhujumu uchumi na kulisababishia taifa hasara ya zaidi ya Sh milioni 657.5
Khane amesomewa mashitaka ya awali ya uhujumu uchumi. 

Mbele ya Hakimu Mfawidhi Mkoa wa Arusha, Agustino Rwizile imedaiwa kuwa mshitakiwa huyo kati ya mwaka 2013 na mwaka 2014, alisababisha hasara kwa kuingiza mitambo ya mawasiliano na kutoza gharama za kimataifa kinyume cha sheria.
Pia mshitakiwa anadaiwa kusajili majina ya kughushi, kuuza mashine za mawasiliano na kumiliki mtambo wa mawasiliano huku akitumia mawasiliano ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) bila idhini ya serikali kujipatia mamilioni ya fedha.
Mshitakiwa huyo amekana mashitaka. Mahakama imemnyima dhamana kwa kuwa mashitaka hayo hayana dhamana.
Kesi hiyo itasikilizwa tena Desemba 16. Upande wa serikali unatarajiwa kulwa na mashahidi kuthibitisha madai yanayomkabili mshitakiwa huyo.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP