Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe pichani

Na Mathias Canal


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU imeeleza kuwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jan tarehe 
07 Desemba, 2016 alifanya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja na Mkuu wa Mkoa 
mmoja na pia amefanya mabadiliko madogo katika Wizara na Mikoa kama 
ifuatavyo;



Dkt.
Magufuli amemteua Prof. Faustin Kamuzora kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya 
Makamu wa Rais.Kabla ya uteuzi huo, Prof. Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu 
Mawasiliano.


Rais
Magufuli amemteua Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara 
ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo. Mhandisi Mathew 
Mtigumwe anachukua nafasi ya Dkt. Frolence Turuka ambaye ameteuliwa kuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.


Kabla
ya uteuzi huo Dkt. Frolence Turuka alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya 
Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliyekuwa akishughulikia Kilimo. Anachukua 
nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Rais
Magufuli amemteua Dkt. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya 
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na atakuwa akishughulikia Mawasiliano. 
Dkt. Maria Sasabo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Faustin 
Kamuzora ambaye ameteuliwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.

Pia
Rais Magufuli amemteua Mhandisi Angelina Madete kuwa Naibu Katibu Mkuu 
Katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Mhandisi Angelina 
Madete anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Maria Sasabo 
aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na 
Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano.


Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.


Wakati huo huo,
Rais Magufuli amemteua Bw. Christopher Ole Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Njombe.Bw. Christopher Ole Sendeka anachukua nafasi ya Dkt. Rehema 
Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa 
Singida.


Dkt.
Rehema Nchimbi anajaza nafasi iliyoachwa na Mhandisi Mathew Mtigumwe 
ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo 
anayeshughulikia Kilimo.





Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Dkt. Osward J. Mashindano kuwa Msajili wa Hazina. 

Dkt. Osward J. Mashindano anachukuwa nafasi ya  Bw. Lawrence Mafuru ambaye atapangiwa kazi nyingine