Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP Ernest Mangu (wapili kulia) akiwaongoza askari na Maofisa wa Jeshi la Polisi katika matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya ya mwili katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Jijiji Dar es salaam leo, kulia ni Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia nchini (DCP) Frasser Kashai, anayefuata ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni (SACP) Susan Kaganda.

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakiwa katika matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya ya mwili yaliyoongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu (hayupo pichani) yaliyofanyika katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni jijini Dar es salaam leo.

 Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya ya mwili yaliyoongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu (hayupo pichani) katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni leo. 

 Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya ya mwili yaliyoongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni (SACP) Susan Kaganda, akipita katikati ya dimbwi la maji maeneo ya Kinondoni Makaburini, yaliyotokana na mvua iliyonyesha mapema asubuhi, wakati akiwa katika matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya ya mwili yaliyoongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangupamoja na askari na mofisa wa Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP Ernest Mangu (wapili kushoto) pamoja na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni (SACP) Susan Kaganda, wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya ya mwili katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni.
(Picha zote na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi)