Image result for KAMANDA WA POLISI
ARUSHA MKUMBO
Kamanda wa
Polisi
Mkoani Arusha Charles
Mkumbo
Na Woinde Shizza,Meru

MWANAFUNZI wa
kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kitefu iliyopo

Meru  mkoani Arusha amenusurika kufa mara baada ya kubakwa na
kuteketezwa
kwenye  korongo la mchanga na
kusababishiwa  maumivu makali
yaliyomsababishia kushindwa
kuendelea na masomo yake kwa muda.



Akielezea tukio
hilo  mwanafunzi huyo ambae amehifadhiwa jina kwa sababu za

kimaadili alisema kuwa tukio hilo lilitokea novembar 13 majira ya saa
12.30
alipotoka kwa kinyozi.

Alisema kuwa ghafla
akiwa anarudi nyumbani alikutana na mtu huyo
aliyemfanyia
kitendo hicho na kuanza kumkaba shingoni na kumziba mkono ili

asitoe sauti na ndipo alipomfanyia kitendo hicho cha ukatili
ambacho
kimemfanyia ashindwe kuendelea na masomo yake vizuri.

"Nilijitahidi sana kupiga kelele ila kutokana na alivyokuwa
amenikaba
shingoni alinifanyia kitendo hiki kikatili ambacho
kimejipelekea nishindwe
kuendelea na masomo yangu kwani baada ya
vipimo nimeonekana aliniumiza
sehemu nyingi ikiwemo hata kifua
changu"alisema mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake mama mzazi
wa mwanafunzi huyo aliyejitambulisha Rambikiaeli
Akyoo
alisema kuwa kutokana na vitendo vya ukatili kukithiri kwa mabinti
zao ni vema serikali ikawa inawachukulia hatua mapema wanaohusika
kwani
tangu akamatwe mtuhumiw huyo na kupellekwa kituoni bado
hajasomewa shtaka
linalomkabili hivyo kufanya wanaohusika na
vitendo hivyo kuona wako sawa
kwa vile hakuna hatua kali
inayochukuliwa mapema dhidi ya matukio hayo

Nae mkuu wa
shule hiyo Nkoe Nicolaus  alisema kuwa tukio hilo limemfanya
mwanafunzi huyo aathirike kisaikolojia kwani tangu afanyiwe ukatili
huo
ameshindwa kiendelea na masomo yake vizuri hivyo anawashauri
wazazi wa
binti huyo kumuhamisha shule hiyo na kumuhamishia
nyingine ili kimbadilisha
mawazo ya kifkra.

Kwa
upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha kitefu tanesco Samweli
Matayo
alikiri kutokea kwa tukio hilo katika kitongoji chake na
kusema kuwa mara
baada ya taarifa walifanikiwa kumtia hatiani
mtuhumiwa aliyetambulika kwa
jina la Wilson  Elias ambae
ndie  aliyehusika na ukatili huo  na kumfikisha
katika
kituo kidogo cha polisi usa river ili kukabiliana na shutuma hizo.

Kamanda wa  polisi  Charles Mkumbo amethibitisha
kukamatwa kwa
mtuhumiwa huyo ambapo limesema
kuwa
mtuhumiwa alikamatwa kwa rb namba RB/R/4250/2016  na
atafikishwa
mahamani upelelezi
ukikamilika.