Mwanamke mmoja raia wa Misri anayeaminiwa kuwa mtu mzito zaidi duniani akiwa na kilo 500, hivi karibuni atasafirishwa kwenda nchini India kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzito wake.
Eman Ahmed Abd El Aty mwenye umri wa miaka 36, atasafirishwa kwa ndege ya kukodishwa kwenda mjini Mumbai, ambapo daktari Muffazal Lakdawala, anapanga kumfanyia upasuaji.

Ubalozi wa India mjini Cairo ulikuwa umemnyima visa kwa kuwa hakuweza kufika kwenye ubalozi huo yeye binafsi.
Hata hivyo hali ilibadilika baada ya daktari kutoka mji wa Mumbia kuindikia kwa wizara ya mashauri ya kigeni ya India kupitia mtandao wa Twitter.
Familia ya bi Abd El Aty inasema kuwa hajaondoka nyumbani kwa miaka 25.
Ikiwa madai kuhusu uzito wake ni ya ukweli basi atakuwa mtu mzito zaidi duniani aliye hai kwa kuwa Pauline Potterraia raia ndiye anashikia rekosi ya Guinness
Alikuwa na kilo 292 mwaka 2010.