NAPE NAUYE AWAPONGEZA TBN KWA UPASHAJI WA HABARI



Dar es Salaam, WAZIRI wa habari na Uenezi, Nape Nauye, amesema siri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuingia madarakani nimitandao ya kijamii.

Akifunga kongamano la mkutano mkuu wa Umoja wa Wanachama wa mitandao ya kijamii(blogeers), Nape alisema CCM imeingia madarakani baada ya kuandikwa kwa upana mkubwa katika mitandao ya kijamii.Alisemamitandao ya kijamii iko na nafasi kubwa katika jamii ambapo asilimia kubwa ya

Watanzania wanatumia mitandao ya kijamii ambapo habari nyingi wakati wa kampeni

walikuwa wakisoma katika mitandao hiyo.

“Leo nitoe
siri kwenu kuwa CCM kuingia madarakani ni ninyi mabloggers, hivyo nawapongezeni
na niko nanyi bega kwa bega” alisema Nauye

Aliitaka
mitandao hiyo kufuata maadili ya upashaji habari na kuepuka upotoshaji jambo
ambalo linaweza kuwa hatari kwa jamii hivyo kuwataka kuzingatia taaluma hiyo.


                                     










Waendeshaji wamitandao ya kijamii (bloggers) wakipiga picha ya Selfie na Waziri
wa habari na Uenezi mara baada ya kufunga kongamano la mkutano mkuu wa mwaka wa
Tanzania Network (TBN) jijini Dar es Salaam leo