Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Dec 27, 2016

Trump: UN ni baraza la kupiga gumzo

Rais mteule wa Marekani , Donald Trump, kwa mara nyengine tena amelikashifu shirika la Umoja wa Mataifa.
Kupitia akauntI yake ya Twitter, amesema shirika hilo linamsikitisha kwa madai kwamba badala ya kuwa shirika lenye hadhi kuu zaidi, limekuwa kama baraza la watu kukusanyika na kupiga gumzo.

Hii ni baada ya jaribio lake la kutaka kupinga azimio lililokemea mpango wa Israel kuendelea kujenga makaazi yao katika ardhi ya Wapalestina kufeli.Baraza la usalama la Umoja wa Matifa limesema kuwa Israel inakiuka sheria za kimataifa kwa kujenga katika ardhi ya Wapelestina.
Azimiio hilo lilipitishwa Ijumaa iliyopita huku Trump akitoa onyo kwamba mambo yatakuwa tofauti wakati atakaposhika rasmi hatamu za uongozi wa Marekani.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP