Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Dec 14, 2016

UN: Boko Haram yasababisha watoto laki nne kukabiliwa na utapiamlo Nigeria

Umoja wa Mataifa umesema kuwa zaidi ya watoto laki nne wanakabiliwa na utapiamlo nchini Nigeria kwa sababu ya mapigano ya Boko Haram na robo yao huenda wakafariki mwakani.
UN imesema wengi wa watoto hao wamedumaa kwa kukosa chakula
Image captionUN imesema wengi wa watoto hao wamedumaa kwa kukosa chakula
Shirika la kuwahudumia watoto duniani UNICEF limetaja sehemu zilizo athirika zaidi kuwa ni jimbo la Borno, huku robo tatu ya maji na pamoja na miundombinu ikiwa imeharibiwa ama kutokuwepo kabisa.
Umeonya kuwa magonjwa ya kuharisha pamoja na malaria yanaongezeka yanayohatarisha zaidi maisha ya watoto.
Boko Haram walianza harakati zao mwaka 2002
Image captionBoko Haram walianza harakati zao mwaka 2002

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP