Vikosi vya usalama nchini Jordan vimetangaza mwisho wa vizuizi katika mji wa kihistoria wa Karak. Taarifa hiyo ilisema vikosi hivyo viliua watu wanne wenye silaha baada ya kuwatoa nje ya ngome hiyo mjini Karak maarufu kwa watalii, huku watu kumi wamekiuawa na wasmambuliaji.

Hata hivyo kati ya watu hao kumi waliouawa yupo mtalii raia wa Canada.
Taarifa ya idara za usalama nchini Jordan zinasema kuwa washambuliaji hao walianza kuwafyatulia risasi polisi waliokuwa doria,huku kukiwa na mkusanyiko wa watu katika eneo hilo la Kihistoria. Polisi wamefanikiwa kuwaua washambuliaji wanne na kufanikiwa kupata vifaa vya milipuko,ikiwemo mikanda ya silaha za kujitoa muhanga.
Hali ya usalama imeendelea kuimarishwa dhidi ya shambulizi jingine lolote linaloweza kutokea.