Pombe nchini UrusiImage copyrightAFP
Image captionPombe nchini Urusi

Takriban watu 41 wamefariki katika mji wa Serbia wa Irkutsk baada ya kunywa sabuni ya kuogea, kulingana na mamlaka ya Urusi.
Sabuni hiyo ilio majimaji ilitumika kama pombe kulingana na kamati ya uchaguzi nchini Urusi. Watu wengine 16 wako katika hali mbaya.
Tayari watu wawili wanazuiliwa kufuatia kisa hicho huku polisi wakionda chupa za sabuni hyo katika maduka.
Wachunguzi wanasema onyo kwamba sabuni hiyo haikufaa kutumika kama kinywaji lilidharauliwa.
Bidhaa hiyo ilikuwa na methanol, kemikali inayotumika kuyeyusha barafu.
Hali ya tahadhari imetangazwa katika eneo hilo la Irkutsk, na wachunguzi wa Urusi wameanzisha uchunguzi.
Vyombo vya habari vya Urusi vimeripoti kwamba waathiriwa walikuwa watu masikini ,walio na umri kati ya 35 na 50 na kwamba hawakuwa wakinywa kwa pamoja.
Bidhaa za nyumbani mara nyengine huonekana kuwa rahisi kwa matumizi mbadala ya pombe katika eneo hilo lililokuwa muungano wa Usovieti.
Huku visa vya sumu ya pombe vikiwa vya kawaida, kisa hiki ndicho kibaya zaidi kuwahi kutokea kwa miaka kadhaa.