Polisi katika jimbo la Florida wanamzuilia mwuaji mshukiwa baada ya watu watano kupigwa risasi na kuawa na wengine wanane kujeruhiwa katika uwanja wa ndege wa Lauderdale.
Shambulizi hilo lilitokea katika eneo la kupokea mizigo. Lengo la shambulizi hilo halijulikani.
Mshukiwa ametajwa kama Estaban Santago aliyepatikana na kitambulisho cha kijeshi na ambaye amewahi kufanya kazi Iraq.
Maafisa wa FBI katika afisi ya Alaska wamekuwa na hali ya wasiwasi kumhusu kwa sababu ya tabia zake za zisizoeleweka na mnamo Novemba walimwelekeza kwa daktari bingwa wa akili.
Polisi wanasema mshukiwa huyo hakusema lo lote kabla ya mashambulizi au baadaye. Alipoishiwa na risasi alilala chine kwa upole.
Mshukiwa alikamatwa akiwa bila silahaImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionMshukiwa alikamatwa akiwa bila silaha
Watu wakitumia magari kujikingaImage copyrightAP
Image captionWatu wakitumia magari kujikinga