Maneno yake ya mwisho aliyoyasema kabla ya kuondoka kwenye Mwezi yalikuwa: "Tunaondoka jinsi tulivyokuja na, Mungu akitujalia, tutarejea na amani na matumaini kwa binadamu wote."
Alikuwa kamanda wa chombo cha anga za juu cha Apollo 17 wakati huo.
Ni watu 12 pekee waliowahi kutembea kwenye Mwezi, na kati yao ni sita pekee ambao bado wako hai.
Haki miliki ya pichaNASA VIA REUTERSImage captionCernan alisafiri anga za juu mara tatu
Kupitia taarifa, familia ya Cernan imesema alifariki dunia Jumatatu baada ya kupata matatizo ya kiafya.
Hawakutoa maelezo zaidi.
Haki miliki ya pichaEPAImage captionCernan alistaafu 1976,
Kabla ya kufanya safari ya Apollo 17, Cernan alikuwa amesafiri anga za juu mara mbili awali - mwaka 1966 na 1969.
Alistaafy mwaka 1976 na akaingilia biashara ya kibinafsi. Alikuwa mara kwa mara akichangia katika runinga kuhusu masuala mbalimbali.
Cernan pia aliandaa makala ya video kuhusu maisha yake.
0 Comments