Na Woinde
Shizza,Arusha





Mfanya biashara maarufu wa madini  jijini Arusha, Venance  Moshi

(30)amefikishwa Mahakamani na kusomewa maelezo ya awali katika kesi

 inayomkabili ya kushambulia na kumjeruhi  mkewe kwa chupa
usoni ,wakiwa

wanasuluhishwa na baba mkwe, mgogoro wa ndoa yao.









Mbele ya hakimu , Devota Msofe wa mahakama ya wilaya .Arusha ,mwendesha

mashtaka wa serikali ,Agnesi Hyera alieleza mahakama hiyo kuwa mnamo
marchi

11 mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa
ndoa

yao ,mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia

mlalamikaji (mkewe) Agnesi Joseph (30)iliomjeruhi vibaya  .





Mwendesha mashitaka aliieleza mahakama hiyo kuwa kuwa hatua hiyo

ilimsabishia mlalamikaji atokwe na damu nyingi na baadae kutoa taarifa

kituo cha polisi ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na baadae kufikishwa

mahakamani.







Baada ya kusomewe maelezo hayo mshitakiwa  huyo alikana mashtaka
,na hakimu

Msofe  alipanga siku ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo,baada
ya upande

wa jamhuri kudai kuwa wapotayari kwa usikilizwaji wa kesi hiyo.







Katika shauri hilo la jinai namba 438 la mwaka 2016 ,upande wa jamhuri

unatarajia  kuwasilisha mashahidi watatu na vielelezo kadhaa
ikiwemo hati

ya polisi(PF3) , hati ya daktari pamoja na picha za jeraha .Kesi hiyo

imepangwa kusikilizwa february  6 ,mwaka huu ,saa tatu asubuhi.







Aidha katika hatua nyingine ,shahidi namba moja wa kesi hiyo ,Agnes Joseph

anatarajia kufungua kesi nyingine ya kudai talaka kwa mumewe huyo

waliyefunga naye ndoa mwaka 2012 baada ya ndoa yao kukumbwa na migogoro ya

mara kwa mara huku akiambulia kipigo na vitisho.







Alisema  ameishi na mumewe huyo katika mazingira ya migogoro na
wamekuwa

wakisuluhishwa mara kadhaa bila mafanikio,