IDADI ya watu waliokufa katika shambulio la bomu la kutegwa kwenye gari kwenye kituo cha kijeshi Kaskazini mwa Mali imefikia watu 50.
Maafisa wamesema shambulio hilo limetokea baada ya lori lilijazwa baruti kulipuliwa kwenye kambi ya waasi wa zamani na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali katika mji wa Gao.
Watu wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio hilo.
Eneo hilo la jangwa Kaskazini mwa Mali limekuwa na vurugu tangu lilipotekwa na wapiganaji wa kiislamu mwishoni mwa mwaka 2012.
Licha ya jeshi la Ufaransa kuingilia kati mwaka 2013 eneo hilo bado halina utulivu huku kukitokea mashambulio ya mara kwa mara na utekaji nyara.
|
0 Comments