Magari
WALIONUNUA magari kutoka nje ya nchi wakauza kwa wengine bila kwenda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kubadilisha umiliki, wajue bado wanadaiwa gharama za leseni ya uendeshaji magari barabarani.
Wanadaiwa kutokana na ukweli kwamba mfumo wa kompyuta wa mamlaka unaendelea kusoma kama wao bado ni wamiliki halali wa magari hayo.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Dodoma, Mathias Masese alisema mjini hapa wamba, kama mtu wameuza gari yake kwa mtu mwingine, anatakiwa kuandika barua kwenye mamlaka hiyo kuonesha kwamba wameliuza.
Meneja huyo alisema hata kama mtu umeuza pikipiki, gari, bajaj au chombo kingine cha usafiri, na hujaandika barua TRA kuomba kubadilisha umiliki, ajue gharama za ulimiki gari litaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka.
Mnunuzi wa chombo chochote cha usafiri, kama umekiuza kwa mtu mwingine, anatakiwa kuandika barua ya kubadilisha jina ili lisomeke la yule uliyemuuzia.
Meneja huyo alisema kama gari limefanywa kuwa chuma chakavu, mmiliki wake aandike barua kuonesha gari hilo halipo na aleke kadi ya gari ili kusimamisha kuendelea deni hilo.
Hata kama gari halipo barabarani kwa miaka mitatu au limepelekwa gereji au limeegeshwa nyumbani, mfumo wa kompyuta ya mamlaka haufuti deni hilo.