Wasuluhishi kutoka maeneo mbalimbali wanaojaribu kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Gambia wameahirisha kwenda nchini humo kutokana na ombi la rais Yahya Jammeh.
Badala yake watakwenda nchini humo siku ya Ijumaa.

Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi wamemtaka Jammeh akubali kushindwa katika uchaguzi uliofanyika mwezi jana, na kuongeza kusema watahudhuria sherehe za kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Adama Barrow baadae mwezi huu.
Mwanzoni, waziri wa habari za Gambia amesema itakuwa kinyume cha katiba kumwapisha Barrow mpaka pale kesi iliyowakilishwa mahakama na bwana Jammeh ya kupinga matokeo itakapoamuliwa.
Kwa upande mwengine, mahakama kuu nchini humo haitaweza kusikiliza kesi hiyo mpaka mwezi Mei mwaka huu, kutokana na ukosefu wa mahakimu.