Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jan 2, 2017

Waziri wa mazingira auawa Burundi

Waziri wa mazingira huko Burundi Emmanuel Niyonkuru, amefariki baada ya kupigwa risasi mjini Bujumbura saa chache tu baada ya kuingia mwaka mpya.
Police wanasema amepigwa risasi alipokuwa akielekea nyumbani kwake eneo la Rohero .
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, ameapa kuchukua hatua kali za kisheria kwa atakayepatikana na hatia ya kuhusika katika mauaji hayo.
Rais wa Burundi PIerre Nkurunziza amesema kuwa waliohusika watachukuliwa sheria kali.

Waziri wa mazingira nchini Burundi Emmanuel NiyonkuruImage copyrightSERIKAI YA BURUNDI
Image captionWaziri wa mazingira nchini Burundi Emmanuel Niyonkuru

Mamia ya watu , wakiwemo maafisa wa ngazi za juu katika jeshi wameuawa tangu rais PIerre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu 2015, hatua ambayo wapinzani wanasema ni kinyume na sheria.
Lakini hii ni mara ya kwanza kwa waziri wa serikali kuuawa.
Kwa miezi kadhaa taifa hilo limekuwa tulivu.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP