Wafanyikazi sita wa shirika la msalaba mwekundu nchini Afghanistan wameuwawa na washukiwa wa kundi la wanamgambo wa Islamic State (IS), katika jimbo la Jowzjan, kaskazini mwa nchi hiyo.
Wafanyikazi hao wote walipigwa risasi na kuuwawa katika eneo la Qush Tepa, gavana wa eneo hilo ameiambia BBC.
Wafanyikazi wengine wawili hawajulikani waliko, huku hofu ikitokea kuwa, huenda wametekwa nmyara. Amesema gavana huyo. Shirika hilo la msalaba mwekundu ICRC limethibitisha mauwaji hayo, lakini halijasema ni nani aliyewauwa.
Kundi la wapiganaji la Islamis State ambalo pia linafahamika kama Dayesh, limekuwepo nchini Afghanistan tangu mwaka 2015.
Kundi hilo limekiri kutekeleza mauwaji ya hivi karibuni mashariki mwa taifa hilo na mjini Kabul.

Januari 2015, kundi la IS lilitangaza kupanua maeneo yake ndani ya Afghanistan hasa mashariki mwa jimbo la mashariki mwa Nangarhar, mpakani na Pakist
Image captionJanuari 2015, kundi la IS lilitangaza kupanua maeneo yake ndani ya Afghanistan hasa mashariki mwa jimbo la mashariki mwa Nangarhar, mpakani na Pakistan

Hakuna taarifa wala kundi lolote ambalo limekiri kuhusika na shambulio hilo la Jowzjan.
Kundi la msalaba mwekundi ICRC limeandika kwwenye mtandao wake wa Tweeter "Tumetamaushwa na kushtuka" na taarifa hizo.
Kiongozi mkuu wa lkundi hilo, Peter Maurer, amesema kuwa hilo ni shambulio la makusudi kwwa wafanyikazi wake na "tunalilaani kabisa".
Shirika la ICRC halijawahi kutatizwa kwa namna yoyote nchini Afghanistan kwa miaka 30 na sasa limesema kwamba litatathmini operesheni yake nchini humo.