Maharusi waliowasisimua wengi baada ya kutumia Sh100 pekee za Kenya kugharimia harusi, wameandaliwa sherehe ya harusi ya kufana jijini Nairobi.
Sherehe hiyo ya marudio imeandaliwa katika bustani ya Eden Bliss, Nairobi ulimwengu ukiandhimisha Siku ya Wapendanao.
Harusi ya Anne na Wilson Mutura ya awali iligharimu dola moja pekee ya Kimarekani lakini sherehe ya sasa inakadiriwa kwamba imegharimu takriban Sh3.5 milioni (Dola 35,000).
Sherehe hiyo ya marudio imeandaliwa katika bustani ya kifahari ya Eden Bliss viungani mwa Nairobi
Pesa hizo zimegharimiwa na makundi mbalimbali yanayohusika katika uandaaji wa sherehe, ambayo yaliungana kwa pamoja na kuchanga pesa kuandalia Anne na Wilson sherehe ya kukata na shoka.
Mmoja wa waandalizi wakuu wa harusi hiyo Aaltonen Jumba kutoka Slique Events Planner Limited, hata hivyo anasema ni vigumu kujua hasa ni kiasi cha peza zilitumiwa kuiandaa.
Ameambia BBC kwamba wahudumu mbalimbali walijitokeza kusaidia kwa kutoa huduma zao, na hakuna pesa taslimu zilizotolewa.
Kuna waliotoa mahema, wengine viti na wengine magari ya kifahari.

Wawili hao wamesafirishwa kwa magari ya kifahariHaki miliki ya pichaAALTONEN JUMBA
Image captionWawili hao wamesafirishwa kwa magari ya kifahari

Kwa sababu walikuwa tayari washafunga ndoa rasmi, kwenye sherehe ya leo, walibadilisha pete zao. Baadhi ya Wakenya mitandaoni wamekuwa wakikosoa uamuzi wa kutumia pesa nyingi kugharimia sherehe nyingine ya harusi kwa wawili hao.
Lakini Bw Jumba anasema wanaokosa sherehe hiyo wamekosa kutambua na kufahamu vyema mambo ambayo yamekuwa yakijiri.
"Wawili hao tayari wamesaidiwa kifedha. Wamepewa shamba la kisasa, wakalipiwa fungate na wameahidiwa pesa za kutumia kama mtaji kuanzisha biashara," alisema.
"Kwa sababu yote yameshughulikiwa, mbona tusiwape kile ambacho walikosa? Kila mtu hutamania sana kuwa na sherehe kubwa ya harusi."

Bw Wilson akisaidiwa kuweka sawa koti lakeHaki miliki ya pichaNDUNGU NYORO / FACEBOOK
Image captionBw Wilson akisaidiwa kuweka sawa koti lake
AnneHaki miliki ya pichaNDUNGU NYORO / FACEBOOK
Image captionBi Anne wakati wa sherehe ya harusi ya marudio

Wawili hao, wanaoishi eneo la Kasarani, Nairobi, walisifiwa kwa kuonyesha thamani halisi ya mapenzi badala ya kuongozwa na pesa.
Kando na kuandaliwa harusi hiyo, wametunukiwa shamba la kilimo cha kisasa, fungate kwenye hoteli ya kifahari na baada ya sherehe ya leo wanatarajiwa kwenda kwa fungate nyingine mjini Dubai.
Dola yenyewe walioyotumia Anne na Wilson katika harusi yao ya mwanzo waliitumia kununua pete mbili.
Walikuwa wameahirisha harusi yao mara tatu baada ya kukosa fedha za kutosha kuandaa sherehe kubwa ya harusi.
Maombi yao kwa familia na marafiki kuwafanyia mchango, hayakutimizwa.
Baada ya muda, Bwana harusi, Wilson, hakuwa na la kufanya ila kumshawishi mpenzi wake kuhusu uwezo wake.
"Wilson aliponieleza hali yake, sikukataa. Mapenzi yetu yalizidi yote," Ann aliambia BBC.
Ingawa walikuwa na uwezo wa kuishi kwa mtindo wa 'come we stay' uliomaarufu kwa vijana wengine ambapo wapenzi wanaishi pamoja bila kuoana, Wawili hao walikwenda kwa askofu Jasper Owach kutoka Kanisa la Community Christian worship centre mjini Nairobi kurasmisha harusi yao.
"Mapenzi yetu yalidumu kwa muda na ili kujistiri kutoka maovu baada ya kupata baraka ya wazazi, tuliamua kufanya mambo yetu rasmi," anasema Wilson.

Wilson Muturi na mkewe Ann
Image captionWilson Muturi na mkewe Ann walitumia dola moja pekee wakati wa harusi yao

Siku yenyewe ilipofika, bwana Harusi, Wilson aliwashangaza waumini baada ya kukimbia nje sherehe ikiendelea.
"Alitoka ghafla kununua pete ya harusi nilipokuwa naendelea na shughuli ya kuwafunganisha," alisema askofu Jasper Owach, ambaye aliongoza hafla hiyo.
Wilson alirejea na walipokuwa wanatamka kauli za ndoa, Wilson alitoa pete hizo zilizofungwa kwa gazeti na wakavikana pete.
Wawili hao, wamewarai vijana kutozuiwa na uwezo wao wa kifedha na hivyo basi kuhalalisha mapenzi yao kupitia ndoa.

MaharusiHaki miliki ya pichaAALTONEN JUMBA