Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza  na waandishi  wa habari (hawapo pichani) juu ya ugeni wa marais wawili kutoka nchi za Uganda na Visiwa vya Shelisheli leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Marais wa nchi mbili wanatarajia kufanya ziara nchini na kufanya mazungumzo na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika masuala ya uchumi pamoja masuala ya uhusiano wa kidiplomasi katika nchi hizo.

Marais hao watakaofanya ziara hiyo,ni Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni  pamoja na Rais wa Visiwa vya Shelisheli, Danny Faure.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ziara hizo zinafaida kwa watanzania katika uchumi.

Rais wa Yoweri Kaguta Museveni anatarajia kuwasili kati ya Februari 25 na kuondoka February 26 na Rais  wa Shelisheli, Danny Faure anatarajia kuwasili February 27 na kuondoka February 28.

Makonda amesema kuwa ziara hiyo inatokana na Mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika  ambapo Rais Dk. John Pombe Magufuli alikutana na baadhi ya marais ambao wametaka kuja kufanya ziara nchini kwa faida katika nchi hizo.
 Amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza katika kuwalaki viongozi hao kama uzalendo uliozoeleka.