MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akimkabidhi mifuko ya saruji kwa ajiri ya ujenzi wa jengo la ofisi ya chama katika kata ya Ruaha kwa mwenyekitiwa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza
 MBUNGE wa viti maalumu Mkoa
wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa katika eneo la uwanja wa kujenga ofisi ya kata ya Ruaha

 MBUNGE wa viti maalumu Mkoa
wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akibadilishana mawazo na katibu wa ccm manispaa ya Iringa Nuru Ngereja
 MBUNGE wa viti maalumu Mkoa
wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa hama hicho wa kata ya ruaha
 MBUNGE wa viti maalumu Mkoa
wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na

mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza pamoja na viongozi wengine wa chama hicho.
 MBUNGE wa viti maalumu Mkoa
wa Iringa Ritta Kabati akipokelewa na wanachama wa mtaa wa kigamboni mkoani Iringa

Na Fredy Mgunda,Iringa.


MBUNGE wa viti maalumu Mkoa
wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) ameanza kusaidia
Ujenzi wa ofisi za Matawi ya CCM katika kata mbali mbali za Jimbo la Iringa mjini
kama sehemu ya majukumu yake ya kukijenga chama hicho ambacho kilipoteza kiti
cha ubunge na halmashauri kuchukuliwa na wapinzani.








Akizungumza wakati wa
kukabidhi mifuko ya saruji kwa Ujenzi wa ofisi za Tawi Kigamboni na Ruaha
,Kabati alisema kuwa anafanya hivyo kama njia ya kutekeleza ilani na maadhimio
ya miaka arobaini ya chama cha mapinduzi.




“Nakipenda chama changu ndio
maana napigana sana kuhakikisha chama cha mapinduzi mkaoni mhapa iringa
kinarudi mahala pake na kuhakikisha kinaaminika kwa wananchi na wanachama
wa  manispaa ya Iringa”.alisema Kabati 





Hata hivyo Kabati alisema
kuwa ataendelea kusaidia Ujenzi wa ofisi hizo ili kuona ndani ya kipindi kifupi
cha miezi mitatu ama sita kila tawi linakuwa na ofisi yake ya tawi na aliwataka
wanachama wa CCM kushikamana na kuendelea na Ujenzi wa ofisi hizo pamoja na
kujihusisha na shughuli nyingine za kijamii








"Haiwezakani chama kikubwa
kama hiki kukosa ofisi za matawi wakati tunamaeneo mengi ya kujenga ofisi
nitakikisha tunashirikiana na wanachama na wananchi wengine kujenga hizo ofisi
ili kumuunga mkono Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DR John Pombe
Magufuli ambaye anapambana kuhakikisha cha mapinduzi kinakuwa chama cha
wananchi wa chini na sio matajiri pekee yao".alisema Kabati





Kwa upande wake mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza aliwataka
wanachama kuwa kusahau yaliyopita na kuanza kujenga chama upya.




“Tulipoteza halmashauri ya
Iringa na jimbo hivyo inabidi tukae chini na tujipange upya kukijenga chama
maana tunajua kwa kujenga ofisi za matawi zitatusaidia kurudisha hadhi na hali
ya chama hapa manispaa kwa kutoa huduma bora kwa wananchi wote bila kuchagua
chama”.alisema Kiponza 





Kiponza alimshukuru mbunge
wa viti maalumu Ritta kabati kwa mchango anaoutoa kwa kuleta maendeleo katika
manispaa ya Iringa hasa ukiangalia ujenzi wa majengo mbalimbali ya
shule,taasisi za kidini,taasisi za kijamii hapa kujenga majengo ya chama.





Lakini Kiponza alimtaka
mbunge Kabati kuwasaidia wananchi wanaodhurumiwa na kunyang’anywa mali zao katika
manispaa ya Iringa.





“Hapa kigamboni kunawananchi
wanapigwa na viongozi wa mtaa kwa kuwa wapo CCM tu na wamenyang’anywa kituo cha
kuchotea maji ambacho kilikuwa mradi wa chama cha mapinduzi hivyo lazima
upambane kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na mali za chama zinarudi
kwenye chama”.alisema Kiponza





 Naye Katibu wa CCM manispaa ya Iringa Nuru
Ngeleja alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha ofisi zote za chama zinajengwa na
zinakuwa katika ubora unaotakiwa kutokana na ukubwa wa chama cha mapinduzi(CCM)
na kuahidi kuwa wataendelea kumuunga mkoano Rais wa jamhuri ya muungano ya
Tanzania Dr John Pombe Magufuri.





“Sisi tunafanyakazi ya
kumsaidia mwenyekiti wetu wa chama ambaye ni Rais wetu kwa kufanya kazi na
kuisimamia serikali kufanya kazi kwa uhakika na kuwafaikia na kuwatumikia
wananchi waliowaweka madarakani mpaka sasa”. Alisema Ngereja