Waziri mmoja wa Morocco amesema kuwa taifa lake halitatambua uhuru wa Sahara ya Magharibi na kwamba atayarai mataifa yanayofanya hivyo kubadili misimamo yao.
Naibu waziri wa maswala ya kigeni nchini humo Nasser Bourita alitoa matamshi hayo katika mahojiano na tuvuti ya Kifaransa ya taifa hilo, Le Desk.
Matamashi yake yanajiri chini ya juma moja tu baada ya taifa la Morocco kurudishwa katika Umoja wa Afrika baada ya kuondoka katika Umoja huo 1984 kufuatia mzozo wa eneo hilo.
Bw Bourita amesema kuwa uanachama wa AU hautabadili msimamo wa Morocco kwamba jimbo la Sahara ya Magharibi ni eneo muhimu la taifa hilo.
Umoja wa Afrika unalitambua eneo hilo kuwa huru.
|
0 Comments