Mwanadiplomasia huyo, alipigwa risasi na kuuwawa ndani ya Ubalozi mjini Karchi.
Kiongozi huyo wa kigeni wa Afghanistan, alipigwa risasi na walinda usalama katika ubalozi wa nchi hiyo, ulioko katika mji wa Karachi, kusini mwa Pakistani.
Vyombo vya habari vya nchi hiyo, vimemtambua mwanamume huyo aliyeuwawa kama katibu wa tatu wa ubalozi huo.

Usalama waimarishwa katika eneo lenye balozi nyingi za kigeniHaki miliki ya pichaAP
Image captionUsalama waimarishwa katika eneo lenye balozi nyingi za kigeni

Taarifa kutoka ubalozi wa Afghanistan mjini Islamabad, haikumtambua balozi huyo, lakini ikasema kuwa mlinda usalama wa kibinafsi alikuwa raia wa Afghanistan.
Hakuna taarifa zozote zilizotolewa kuhusiana na nia ya shambulio hilo.
Afisa mmoja wa polisi, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba, mlinzi huyo amekamatwa.