Nchi tano barani Afrika zimekubaliana kuunda kikosi cha pamoja, kupambana na ugaidi katika eneo la Sahel.
Uamuzi huo umetolewa katika mkutano wa mataifa yanayojiita G5: Mali, Chad, Burkina Faso na Mauritania.
Mkutano huo umefanyika baada ya shambulio la mwezi uliopita katika mji ulioko kaskazini mwa Mali, wa Gao, lililosababisha vifo vya karibu watu themanini.
Rais wa Niger Mahamadou Issoufou amesema wataomba idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kabla ya kuundwa kwa jeshi hilo.
Bado hakuna taarifa zozote zilizotolewa juu ya wanajeshi wangapi watahusishwa au makazi ya jeshi hilo.
|
0 Comments