Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Mahakama kukusanya Shilingi Trillioni 7.3 ambazo ni matokeo ya serikali kushinda kesi mbalimbali za ukwepaji kodi.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria na Mwaka mpya wa Mahakama iliyobeba kauli Mbiu isemayo Utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.
Alisema kuwa Takwimu zinaonesha kuwa kumekuwa na baadhi ya kesi za pingamizi za kodi ambapo Serikali imeshinda kesi hizo japo fedha hizo hazijakusanywa mpaka sasa.“Kukwepa au kutolipa kodi ni kosa kubwa sana, kila mtu anawajibu wa kulipa kodi nchini kwa maendeleo ya nchi” nalifafanua Dkt Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa katika kuelekea ukuaji wa uchumi, Mahakama iwe sehemu ya chanzo cha pato la taifa kwa kwa kuhakikisha wale wanaotakiwa kulipa fidia baada ya kushindwa kesi wanafanya hivyo pamoja na kuwabana wakwepa kodi kwani kutimiza hilo kutaleta mabadiliko katika uchumi wa nchi.Na Beatrice Lyimo - MAELEZO.
|
0 Comments