Wanahabari mkoa 
wa  Iringa  walioshiriki  warsha ya siku  moja ya gesi asilia  wakiwa
katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya  Iringa Richard Kasesela wa
tatu  kutoka  kushoto na wawezeshaji wa  warsha hiyo  kutoka
TPDC,warsha iliyofanyika  ukumbi wa  VETA  Iringa kwa  kushirikisha 
wanahabari kutoka mkoa  wa  Njombe ,Ruvuma na wenyeji  Iringa.

 Wanahabari mkoa 
wa  Njombe   walioshiriki  warsha ya siku  moja ya gesi asilia  wakiwa
katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya  Iringa Richard Kasesela wa
tatu  kutoka  kushoto na wawezeshaji wa  warsha hiyo  kutoka
TPDC,warsha iliyofanyika  ukumbi wa  VETA  Iringa kwa  kushirikisha 
wanahabari kutoka mkoa  wa  Njombe ,Ruvuma na wenyeji  Iringa 



Wanahabari mkoa  wa  Ruvuma   walioshiriki  warsha ya siku  moja ya gesi
asilia  wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya  Iringa
Richard Kasesela wa  tatu  kutoka  kushoto na wawezeshaji wa  warsha
hiyo  kutoka TPDC,warsha iliyofanyika  ukumbi wa  VETA  Iringa kwa 
kushirikisha  wanahabari kutoka mkoa  wa  Njombe ,Ruvuma na wenyeji 
Iringa 
 Meneja mahusiano wa
Shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi Tanzania Maria
Mselemu (TPDC)  akitoa  neno wakati wa utangulizi wa warsha hiyo kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma.

Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela amelipongeza Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC) kwa kuendesha mafunzo maalum kwa waandishi wa Habari wa
Mikoa ya Arusha, Iringa,Ruvuma na Njombe  ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo
ya siku moja ambayo yamefanyika mwezi wa pili tarehe ishirini na moja mwaka
huu(21 / 02 /2017) katika ukumbi wa Chuo cha VETA mkoani Iringa.

“Ingawa mafunzo ni mafupi lakini napenda kulipongeza Shirika letu la Mafuta la
Taifa kwa kuona umuhimu wa vyombo vya habari katika kupata uelewa mpana wa
Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi ili waweze kuhabarisha na kuelimisha watanzania
kwa ujumla ili watambue shughuli za shirika na faida zake haswa katika uchumi
wa nchi”, alieleza Mkuu wa Wilaya.


Aidha Mh Kasesela amewaomba Waandishi wa Habari kuwa wazelendo katika kuisaidia
Serikali kutekeleza miradi mbalimbali yenye maslahi mapana katika maendeleo ya
nchi yetu.



‘’Waandishi Wahabari mnapaswa
kuisaidia Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye tija kwa
uchumi wa Taifa, mfano katika vita ya kiuchumi ya kugombania mradi wa bomba la
mafuta ghafi kutoka Uganda kati ya Tanzania na Kenya, wenzetu Kenya
walijitahidi kuandika habari zenye kutoa wasifu wa nchi yao ili kuisaidia
kupata mradi huo, hivi ndivyo mnavyopaswa kufanya kazi kiuzalendo.”


Aliongeza kuwa leo hii mmeweza kuifahamu TPDC sasa mnapaswa kuwaeleza wananchi
miradi inayofanywa na Shirirka hili na manufaa yake katika uchumi wa Taifa,
mwende mkatafiti namna mradi wa bomba la mafuta utakavyonufaisha wananchi
wanaoishi kando ya njia ya bomba hilo, vilevile namna bomba hilo
litakavyosaidia kukuza uchumi wa nchi, hivi ndivyo tunavyoweza kujenga nchi
yetu kupitia taaluma ya uandishi wa habari.


Kasesela alisisitiza kuwa ili tujenge Taifa imara ni vyema tuandike habari kwa
weledi, uzalendo huku tukiondoa tofauti zetu za kiitikadi ziwe za kikabila,
kisiasa au kidini kwa namna hii tutaweza kuandika habari zenye kujenga nchi
yetu na si vinginevyo.

Alisisitiza vile vile juu ya utoaji
taarifa mapema pale mtu anapoona kuna hujuma au uharibifu wa aina yoyote katika
miundombinu hii, akiongea katika warsha hiyo alisema “miundombinu hii ya gesi
na mafuta ni mali ya watanzania hivyo kuilinda ni jukumu letu sote kama
wazalendo wa nchii hii”.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa
warsha hiyo, Afisa mahusiano wa
Shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi Tanzania Maria
Mselemu alisema
warsha hii inalenga kuendelea kuwajengea uwezo zaidi waandishi wetu wa habari
kuweza kuripoti kwa umahiri na ustadi habari za mafuta na gesi.

Mselemu aliwashukuru waandishi wa habari kwa juhudi zao za kuupasha
habari umma na kuwaasa kwamba kalamu yao ina nguvu hivyo ni vyema ikaendelea
kutumika kujenga uchumi wa Taifa kwa kutoa taarifa sahihi kila wakati.


Katika taarifa yake Faustin Kayombo kutoka mkondo wa
juu (TPDC)
alisisitiza juu ya matarajio yasiyo
halisia yaliyopo miongoni mwa wanajamii na kuwaomba waandishi wa habari
kusaidia kuwaeleza wananchi juu ya uhalisia wa sekta.

Kayombo alisema kwamba uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi ni
wa gharama kubwa na hata mafaniko kwa maana ya mapato makubwa kwa Serikali
huchukua muda mrefu kuonekana.                                                                                                                                                                                           
                                                                                                                               

Akitolea mfano mradi mkubwa wa kusindika gesi asilia (Liqufied Natural
Gas-LNG), Kayombo alifafanua kwamba itachukua takribani miaka 8 hadi 10 kabla
ya mzigo wa kwanza wa LNG kusafirishwa kwenda katika soko la dunia kwa mauzo.
Hata hivyo Kayombo alisisitiza
juu ya ushiriki wa wazawa katika sekta hii hususan katika kutoa huduma na kuuza
bidhaa.

Naye mwanasheria wa TPDC  Barnabas Mwashambwa alisema sheria mpya ya
petroli ya mwaka 2015 inawataka wawekezaji wote kutumia bidhaa zinazozalishwa
hapa nchini na kama ikitokea bidhaa hizo hazipo nchini basi kampuni iingie ubia
na kampuni ya kizawa ili kuweza kutoa huduma inayohitajika.
Sheria imeeleza kwamba ubia huo
lazima umpe mzawa ushiriki usiopunguza asilimia 25%, hii ni fursa kwa wazawa na
ni vyema ikachangamkiwa.




Hata hivyo Mwenyekiti wa Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa frank leornad ameliomba
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kutenga muda wa kutosha zaidi
katika uelimishaji ili walengwa waweze kuelewa vyema sekta, ombi ambalo
liliungwa mkono na Mkuu wa Wilaya.


Katika mafunzo hayo waandishi wa habari walipata fursa ya kujifunza kuhusu
maendeleo ya Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi, Matumizi ya Gesi Asilia na Faida
Zake, Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanga na
Usambazaji wa Gesi Asilia Majumbani, Viwandani na kwenye Vituo vya Kujaza
Magari. 
TPDC
imeendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ikiwa na lengo la kuongeza uelewa
zaidi katika sekta hii mpya na changa ya mafuta na gesi hapa
nchini.