Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na marais wa Nigeria Muhammadu Buhari pamoja na Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
Rais Zuma anatarajiwa kupigiwa simu na Trump kwa mujibu wa akaunti ya twitter kutoka ofisi yake.Utawala nchini Nigeria bado haujathibitisha ikiwa kutakuwa na mazungumzo kati ya Buhari na Donald Trump.
Buhari mwenye umri wa miaka 74 ameongeza uwepo wake nchini Uingereza, huku kukiwa na hali ya wasi wasi nchini Nigeria kuwa huenda afya yake ni mbaya.
0 Comments