Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Mexico Luis Videgaray mjini Mexico, mkutano ambao kwa kiasi kikubwa ulitawaliwa na masuala ya sera za uhamiaji.

katika mkutano huo, Waziri wa mambo ya nje wa Mexico, Luis Videgaray, ameonyesha kuchukizwa kwake na Sera za Marekani dhidi ya nchi yake.
Amemueleza US Secretary of state, Rex Tillerson na mkuu wa masuala ya usalama , John Kelly kuwa mapendekezo ya marekani kuhusu masuala ya uhamiaji yana madhara.
Alikua akikosoa mpango wa Marekani kuwarejesha makwao wahamiaji waishio Marekani bila vibali bila kujali raia wa Mexico au la.
''ni heshima kubwa na tunatoa shukrani kwa ujio huu, kwa kuwa umefanyika kipindi kigumu kwa Mexico na Marekani.kama nyote mjuavyo, kumekuwa na hali ya kutoridhishwa ,hali ya kukerwa na kile kinachoelezwa kuwa sera ambazo zinaweza kuleta athari kwa maslahi ya raia wa Mexico ndani na nje ya Mexico''
Kwa upande wake bwana Kelly amesema hakutakuwa na zoezi la kuwarejesha makwao raia wa kigeni waishio kinyume cha sheria nchini Marekani na kuwa jeshi halitatumika kwenye operesheni ya kuwarudisha nyumbani.Amesema hatua zote zitachukuliwa kwa kufuata Sheria
Naye Rais wa zamani wa Mexico, Vicente Fox ameonyesha wasiwasi wake kuhusu utawala wa Trump kuwa umeharibu mahusiano mazuri yaliyokuwapo kati ya Mexico na Marekani
Maafisa hao wawili pia walikutana na Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto, ambaye hivi karibuni alisitisha safari yake ya kukutana na rais wa Marekani,Donald Trump, baada ya Trump kusisitiza kuwa Mexico ilipe gharama za kujenga ukuta wa mpaka baina ya Marekani na Mexico.