Aliyekuwa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na mbunge wa Mtama Nape
Mosses Nnauye amewataka Watanzania kukubaliana na suala la kusitishwa
kwake uteuzi wa cheo hicho baada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
John Magufuli amemteua Dk Harrison Mwakyembe kuchukua nafasi hiyo ya
Nape.

Akizungumza
na waandishi nje ya Hoteli ya Protea leo, Nape amesema wanatakiwa
kukubaliana na hali halisi kwani uteuzi uliofanywa huwezi kuukosoa na
anashikuru kwa kuweza kupata muda wa kufanya kazi na Rais Magufuli.

“Wanachi
mnatakiwa kukubaliana na maamuzi yaliyofanywa na Rais wetu kwani
tukumbuke kuwa Tanzania ni kubwa kuliko Nape na maamuzi yaliyofanywa
yana tija kubwa sana kwa tasnia ya habari, michezo na wasanii na
hampaswi kuanzisha matatizo, Tanzania ni nchi yetu sisi na tujue Nape
hawezi kuwa mkubwa kuliko Tanzania,"

Nape
amesema kuwa anawashauri watanzania wote kuwa watulivu na zaidi
amefurahi kufanya kazi kama Waziri wa habari na amewaomba wana tasnia ya
habari ya habari kushirikiana na Waziri Mteule Harrison Mwakyembe kwani
ni mwanahabari na pia ni mwanasheria mzuri.

“Nina
amini nilitumia akili zangu zote na kwa akili nawashukuru wasanii,
waandishi, wanamichezo kwa ushirikiano wenu. Nilipenda kuendelea kufanya
kazi nanyi lakini muda wa aliyeniteua umefika, nitawakumbuka sana,
ninawapenda sana ila ninawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe na
kuendelea kumwamini Rais wetu John Pombe Magufuli kwani ndiye tuliyepewa
na mungu, ndiye rais tuliyemchagua,” amesema Nape.