Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma hakuhudhuria mazishi ya mwanaharakati wa kuipinga serikali ya ubaguzi wa rangi Ahmed Kathrada kwa ombi la familia yake.
Bwana Kathrada alimtaka Zuma ajiuzulu mwaka uliopita, kufuatia kashfa za ufisadi.
Makamu wa rais Cyril Ramaphosa aliiwakilisha serikali kwenye mazishi hayo.
Bwana Kathrada mwenye umri wa miaka 87, aliaga dunia siku ya Jumanne. Alifungwa pamoja na Mandela kwa kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi.
Alitumikia kifungo cha miaka 26 gerezani kabla ya kauchiliwa mwaka 1989. Baadaye alihudumu kama mshauri ra rais wa zamani Nelson Mandela, kwenye serikali ya kwanza iliyochaguliwa kidemokrasia.
Bwana Zuma alikuwa ameagiza bendera kupepea nusu mlingoti kufuatia kifo chake, na kuhairisha mkutano wa mawaziri ili maafisa wapate kuhudhuria mazishi yake.
Haki miliki ya pichaAPImage captionBwana Zuma amekataa kujiuzulu
Hata hivyo Zuma hakudhuria mazishi wala ibada ya maombi kufuatia ombi la familia ya kathrada.
Mke wa Kathrada Barbara Hogan anafahamika kuwa mkosoaji mkubwa wa bwana Zuma.
Bwana Kathrada alimtaka Zuma ajiuzulu baada ya mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini, kuamua kuwa alikuwa amekiuka katiba kwa kukataa kulipa pesa ambazo zilitumiwa kukarabati makao yake ya kibinafsi huko Nkandla.
0 Comments