Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeandaa hafla maalumu ya
kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya timu ya Serengeti Boys
inayojiandaa kucheza fainali za kuwania Kombe la Afrika kwa vijana wenye
umri chini ya miaka 17 nchini Gabon. Fainali hizi zitafanyika kufanyika
kuanzia Mei 14 hadi 28, 2017. 

TFF inatambua kuwa wadau
mbalimbali wamekuwa wakichangia timu hiyo kupitia mitandao ya simu kama
vile namba 0687 333 222 kadhalika Selcom kwa namba 22 33 44 pia kuweka
fedha kwenye akaunti Na. 00 866 280 03 katika Benki ya Diamond Trust
(DTB).

Sasa siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017 TFF imeandaa hafla
maalumu ya kupokea michango hiyo, lakini pia kuchangisha fedha zaidi
maana lengo ni kukusanya shilingi bilioni moja (Sh. 1 Bil.) Hafla hiyo
itafanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam kuanzia saa moja
jioni.

TFF imeamua kutumia fursa kuwakaribisha wawakilishi wa
makundi mbalimbali ili wawasilishe michango yao na kumkabidhi mgeni
rasmi.

Kwa kutambua michango mbalimbali ambayo imekusanywa
kupitia makundi ya mitandao ya jamii kama WhattsApp, facebook hivyo TFF
inaomba wawakilishi wa makundi yote ya mitandao ya jamii (admins) ambao
wamekusanya michango hii wajiorodheshe ili wapate fursa ya kukabidhi
michango ya makundi yao kwa mgeni rasmi katika hafla hii.

Admins hawa wanaombwa wajiorodheshe kwa kutuma email kwenda fdf@tff.or.tz,
kwa kupiga simu 0787 176767 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda 0787
176767 ambayo pia inapatikana kwenye mawasiliano ya WhattsApp.

Aidha
wawakilishi wa makundi mengine kama idara za Serikali, mashirika ya
umma na binafsi kadhalika watu binafsi ambao nao wamechangia nao pia
tunaomba wajioredheshe ili wapewe fursa pia ya kukabidhi michango yao
siku hiyo ya Ijumaa.

TFF inashukuru sana kwa ushirikiano.

Mungu Ibariki Tanzania

Mungu ibariki Serengeti Boys