Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Apr 7, 2017

Rais wa Somalia atoa msamaha kwa al-Shabab

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi "Farmajo" ametangaza vita dhidi ya kundi la wanamgambo la al-Shabab.
Ametoa pia msamaha wa siku 60 kwa wanamgambo hao, akiwataka kujisalimisha, ili wapate mafunzo, ajira na elimu.

Hi ni baada ya shambulizi la kujitoa mhanga kutokea karibu na jengo moja la serikali mjini Mogadishu ambapo watu 7 waliuawa pamoja na misururu ya kutekwa nyara kwa wafanyakazi wa kutoa misaada katika taifa hilo linalokumbwa na ukame.
Mashambulizi yamekuwa ya mara kwa mara na vikosi vyote nchini Somalia vimekuwa katika hali ya tahadhari ili kukabiliana na tisho lolote kwa usalama.
Pia amesema kuwa amewafanyia mabadiliko maafisa wa vyeo vya juu kwenye idara ya ujasusi na polisi ili kujiandaa katika vita dhidi ya al-Shabab.
Rais ametangaza pia msamaha wa siku 60 kwa wanamgambo hao, akiwataka kujisalimisha, ili wapate mafunzo, ajira na elimu.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais ametangaza pia msamaha wa siku 60 kwa wanamgambo hao, akiwataka kujisalimisha, ili wapate mafunzo, ajira na elimu.


Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP