Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 4, 2017

Cristiano Ronaldo aweka rekodi Instagram

Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji soka wa kwanza duniani kutimiza wafuasi 100 milioni katika mtandao wa kijamii wa Instagram.
Aliandika historia nyingine wiki hii, baada ya kufunga hat-trick yake ya 47 katika uchezaji wake wa soka ya kulipwa.

Mchezaji huyo kutoka Ureno pia ana mashabiki wengi zaidi kwenye Instram kuliko mwanamume mwingine yeyote yule.
Ndiye wa sita katika kufuatwa na watu wengi zaidi mtandao huo duniani.
Wanaomzidi pekee ni Beyonce, Taylor Swift, Ariana Grande, Selena Gomez na akaunti yenyewe ya Instagram.
Ronaldo ana wafuasi wengi kuwashinda Kim Kardashian, Jenner, Justin Bieber na Dwayne 'The Rock' Johnson.
Katika soka, anayemfuata ni nyota wa Barcelona Neymar aliye na wafuasi 74m.
Lionel Messi anakaribia kutimiza wafuasi 71m, David Beckham ana 36m na James Rodriguez ana 30m.
Ronaldo sana hupakia picha zake akiwa mazoezini, akipigwa picha za mitindo ya mavazi na mara kwa mara akiwa na suruali ya ndani au mavazi ya kuogelea.
Ronaldo na mwanaweHaki miliki ya pichaINSTAGRAM
Image captionRonaldo na mwanawe
Lakini picha zake akiwa na mwanawe wa kiume ni miongoni mwa zile maarufu zaidi.
Picha za wawili hao mara nyingi hupendwa na zaidi ya watu milioni tatu.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP