Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisikiliza malalamiko ya wananchi wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam wakielezea adha wanayokumbana nayo kutokana na uharibifu wa Daraja

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori  sambamba na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Ally wakikagua daraja lililovunjika eneo la Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam.
Muonekano wa Daraja la Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam likiwa limeharibika
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam
 
Na Nasri Bakari, Dar es salaam

Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori Leo Jumamosi, Mei 20, 2017
ameagiza kujengwa kwa daraja  jipya kutokana na kuharibika kwa daraja la
awali katika eneo la Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam.

Agizo
hilo amelitoa mapema hii leo wakati akizungumza Na wananchi
waliojitokeza katika mkutano wa Hadhara uliowajumuisha pia Mtendaji wa
Kata,  wajumbe wa mitaa na wataalamu mbalimbali kutoka Manispaa ya
Ubungo.

Mhe Makori amesema kuwa
amejionea adha  iliyopo katika daraja hilo ambapo sio ubovu wa
miundombinu pekee bali pia ni swala la usalama hasa kwa watoto wanaopita
katika daraja hilo waendapo shuleni na sehemu mbalimbali.

"Mimi
kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika Wilaya hii
sitojisikia vizuri kuona tunahatarisha maisha ya binadamu kwa namna
yoyote ile, lazima nihakikishe mnakuwa salama wakati wote" 

"Hivyo
nakuagiza Mkurugenzi kuanza haraka ujenzi wa daraja hili ambalo kwa
kiasi kikubwa litasaidi wananchi Wetu hawa  kupita kwa usalama zaidi"
Alisema Mhe Makori.

Aidha amesisitiza
kuwa kodi zinazokusanywa na serikali  ni kwa ajili ya kugharamia na
kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kama vile
kuboresha Sekta ya Elimu, Afya na huduma nyingine za kijamii, hivyo ni
lazima  serikali ishughulikie na kusimamia mahitaji ya Msingi kwa
wananchi wake.

Sambamba na hayo pia
Mhe Makori amewaomba wananchi kufika kwa viongozi wao pindi wanapopata
kadhia mbalimbali zinazowasumbua katika jamii inayowazunguka kwani
wameajiriwa kwa ajili yao na serikali ya awamu ya tano inajali wananchi
wote hususani wanyonge.

Kwa upande
wake Injinia wa Ujenzi Manispaa ya Ubungo Ndg Goodluck Mbanga amesema
kuwa daraja lililokuwa limejengwa awali lilikuwa Dogo ukilinganisha Na
wingi wa Maji Jambo lililopelekea kuharibika haraka.

Mbanga
Alisema utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Wilaya nitaanza haraka
iwezekanavyo ili kufikia mwanzoni mwa mwaka 2018 lianze kutumiwa Na
wananchi hao ambao wamepata adha kubwa kwa muda mrefu.

Naye
Mwenyekiti wa Mtaa wa Msumi Ndg Hemed Abdallah Gulamu amempongeza Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo kwa Kazi kubwa anayoifanya tangu alipoteuliwa
kuongoza Wilaya hiyo.
Pia amempongeza Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa ufanisi katika
utendaji Na kusema kuwa uongozi wake utaacha alama kubwa na kukumbukwa
na watanzania wote.

MWISHO