Abiria wanaotumia shirika la ndege la Uingereza (British Airways) wameendelea kukwama baada ya kukosekana kwa huduma za ndege hizo.
Katika uwanja wa Heathrow uliopo mjini London, zaidi ya robo tatu ya safari za ndege hizo zilikatiza safari zake.
Kwenye mji wa Rome nchini Italia, abiria wamesema wanapaswa kusubiri mpaka siku ya Jumanne ili kuweza kurejea London.
Shirika hilo linatarajia kuwalipa maelfu ya abiria waliopatwa na usumbufu huo.
Taarifa ya shirika hilo inasema usumbufu huo umesababishwa na kushindwa kufanya kazi kwa mitambo yake ya kutoa mawasiliano siku ya Jumamosi na tatizo hilo linashughulikiwa kwa haraka.
0 Comments