0peresheni kubwa ya kuwaondoa wakaazi wengi wa mji wa Hanover ulioko kaskazini mwa Ujerumani, inaendelea, ya kuwahamisha zaidi ya watu elfu 50 baada ya mabomu makubwa ya wakati wa vita vya dunia, kupatikana kama hayajalipuka.

Wakaazi hao wanatarajiwa kuondoka majumbani mwao baadaye leo, ili kuwapa nafasi wataalamu wa kutegua mabomu, kuhamishia mahala salama mabomu hayo ambayo yanakisiwa kuwa matano.
Operesheni hiyo itachukua siku nzima, na hata zaidi ikiwa mabomu mengineyatapatikana.
Washambuliaji walivamia mji wa Hanover mara 125 kwa mabomu, wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia.
Wataalamu wanaamini kuwa mabomu ambayo hayakulipuka huenda yako chini ya jengo hiliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWataalamu wanaamini kuwa mabomu ambayo hayakulipuka huenda yako chini ya jengo hili
Zaidi ya asilimia 20 ya mabomu yaliyoangushwa mjini humo hayakulipuka.
Baadhi ya mabomu mengine yalikuwa na vifaa vinavyochukua muda mrefu kulipuka, na ambayo kwa sasa yameanza kuoza, na kusababisha hatari kubwa.