Timu ya soka ya Mali iliyo chini ya miaka 17 imeichabanga Ghana kwa goli 1-0 na kufanikiwa kunyakua kombe la mataifa ya Afrika nchini Gabon.
Momadou Samake aliifungia Mali goli hilo pekee na la ushindi.

Baada ya kuingia katika fainali hizo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12, kocha wa Ghana Paa Kwesi Fabin alipanga kikosi chake cha kwanza ambacho kiliifunga Niger 6-5 katika hatua ya penalti kwenye hatua ya nusu fainali.
Ghana walianza kwa kasi kipindi cha kwanza baada ya Eric Ayiah kupata nafasi ya wazi lakini hakuweza kufunga.
Kocha wa Ghana Ghana Paa Kwesi Fabin amesema pamoja na kupoteza mchezo huo, wachezaji wake walifanya jitihada za kutosha ila bahati haikuwa upande wake.