Hotuba ya mkurugenzi wa shirika la ndege la Australia Airline Qantas ilisitishwa kwa muda baada ya kupigwa na chapati usoni.
Alan Joyce alikuwa akihutubia mkutano wa biashara katika eneo la Perth wakati mtu mmoja alipopanda jukwaani na kumpiga chapati ya uso.

Mtu huyo alikamatwa na maafisa wa usalama .
Maafisa wa polisi wanasema kuwa wanamuhoji.
Bwana Joyce alikuwa akizungumza kuhusu hatua ya safari ya moja kwa moja kutoka London hadi Perth bila kusimama katika vituo vilivyopo.
Alan Joyce wa shirika la ndege la Australian QantasHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAlan Joyce wa shirika la ndege la Australian Qantas
''Sijui hilo lilisababishwa na nini '',aliwaambia takriban watu 500 waliokuwa wakisikiliza hotuba yake.
Bwana Joyce aliondoka katika jukwaa hilo kwa muda ili kusafisha uso wake kabla ya kurudi akishangiliwa.
''Sasa iwapo kuna chapati nyengine tafadhali malizeni shughuli yake'', alisema.