Raia nchini Uganda wamekuwa wakisambaza mahojiano ya hivi karibuni ya rais Museveni na shirika la habari la Aljazeera ambapo alizungumzia maswala kadhaa.
Katika mahojiano hayo, alitetea kipindi chake cha miongo mitatau kama rais wa Uganda na kuwashutumu wale wanaomuita dikteta, akisema kuwa huenda amekuwa dikteta mzuri kwa sababu amekuwa akichaguliwa na wananchi mara tano.

Alizungumzia kufungwa kwa mwanaharakati Stella Nyanzi ambaye anazuiliwa kwa kumuita, ''makalio'' akisema kuwa hana haki ya kuwatusi wengine.
''Iwapo wewe ni mwanaharakati na unafanya makosa ,kwa sababu katika kupigania haki za binaadamu pia unafaa kuzungumzia haki za wengine, huwezi kuvunja haki za wengine na kusema kuwa ni haki yako kuwatusi watu hapana.Haki zinaenda sambamba na majukumu, iwapo unajua chochte kuhusu demokrasi. Alikataa kuingizwa katika mazungumzo ya vita vilivyokuwa katika jimbo la magharibi la Kasese,ambapo vikosi vya usalama vilikabiuliana na walinzi wa mfalme wa eneo hilo, mzozo uliowacha makumi kufariki na wengine wengi kuuawa akisema kuwa ni swala ambalo linaangaziwa mahakamani''.
''Swala hilo liko mahakamani na kulingana na mahakama, wakati kitu kinapokuwa mahakamani sifai kuzungumzia. Mahakama itatuambia iwapo watu hao walikamatwa kwa sababu fulani ama la''.