Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemshauri waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ajiuzulu.
Hii leo Magufuli alikua akipokea taarifa ya kamati maalum aliyoiunda kuchunguza mchanga wa madini uliokuwa katika makontena zaidi ya 200 aliyoyazuia yasisafirishwe, kwa ajili ya uchunguzi.

Katika hatua nyingine Magufuli amevunja Bodi ya wakala wa ukaguzi wa madini Tanzania TMAA na kumsimamisha kazi Mkurugenzi wake kwa kushindwa kutimiza majukumu yake.
Ripoti iliyowasililishwa katika ikulu ya Tanzania, iliwasilishwa na kamati ya wataalam wa sekta ya madini kubaini aina na kiwango cha madini yaliyo ndani ya mchanga unaosafirishwa kwenda nje.
Katika makontena zaidi ya 200 yaliyokuwa yakichunguzwa, imebainika kuwa yalikuwa na dhahabu yenye thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni moja za Tanzania.