Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 22, 2017

STAM NA ALLY QWIDO WALIPOFANYA DUA MAALUMU YA KUWAOMBEA WAZAZI WAO ANTWERPEN- PART 2

Ally Qwido pichani akitoa shukrani za dhati kwa niaba yake na mwenzake Stam waliyoiandaa shughuli hii rasmi kwa ajili y kuwaombea wazazi wao waliotangulia mbele ya haki siku chache zilizopita.Dua ilifanyika jana mjini Antwerpen nchini Ubelgiji.

Wungwana mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali barani ulaya walishiriki vyema katika dua ya kuwaombeaa wazazi wa wenzetu waliotangulia mbele za haki.

Mawaidha na nasaha zilizokuwa zikitolewa na mashekh wetu SHekh Hassan na Shekh Habib yaliwagusa kila mmoja wetu

Jungu kuu halikosi ukoko..Idara hii ilikamilika,kiukweli kila mmoja alikifurahia chakula na watu wote walishiba vizuri..

Brother Zile akiwa na kijana wake mikononi,huku shabiki namba moja wa Chelsea Salum Meja toka Holland mwenye fulana ya Bluu akiwa makini kusikiliza mawaidha

Malaika wa Mungu nao walikuwepo


Wakati mawaidha yakiendelea kila mmoja alikuwa makini kusikiliza 

Shekh Habib akiendeleza ukumbusho wa mambo muhimu kuhusu suala zima la umauti kwa mwanandamu

Al habib Ally Qwido akiendeleza yake kwa uchache zaidi,aliwashukuru sana watu wote waliohudhuria shughuli hiyo
Wakati wa sadaka ulipowadia kila mmoja alishiriki zoezi hili la kuweka tumbo sawasawa

 Mahanjumati yakiendelea kupakuliwa na waungwana

 Alhamdulillah chakula kilikuwa kitamu

Dada yetu kipenzi Da' Ummy alihakikisha kila kitu kinakwenda juu ya mstari

 Picha zote na maelezo toka Maganga One Blog.
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP